HALMASHAURI ya Msalala wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, imezindua Siku ya Wanawake Duniani, kwa kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo vitakavyowaweza kuwapa mikopo inayotolewa na serikali kupitia benki ya NMB
Uzinduzi huo umefanyika katika kijiji na kata ya Bugarama kwa kuhusisha wajawasiriamali wa makundi yote, iliyoendana na uhamasishaji wa kupima afya, upandaji wa miti ili kutunza mazingira, kutumia nishati safi, elimu ya mlipa kodi na namna ya kupata huduma kupitia Tanesco.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Glory Absalum, akikabidhi vitambulisho hivyo amesema, kila mjasiriamali anawajibu wa kuwa na kitambulisho hicho, ili kuepukana na usumbufu wanapofika watu wa Mamlaka ya Mapato, sehemu ya biashara au idara ya biashara ya halmashauri.
Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi, kiuchimi wa halmashauri hiyo, Julius Tungura, amesema ya wajasiriamali 21 wamepewa vitambulisho hivyo na wanaendelea kuwaandikisha wengine kwani vinawasaidia kutosumbuliwa kwenye biashara zao.
Amesema, sifa ya kitambulisho hicho ni kumtambulisha rasimi mjasiriamali, kupata maeneo ya kufanyiabiashara zake, mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri pamoja na mikopo.
Mmoja wa wajasiriamali walipokea vitambulisho hivyo, Stella John, fundi cherehani amesema, mpaka sasa ananufaika na mikopo wa asilimia 10 kutoka halmshauri na biashara yake ya kushona inampatia kipato, kwa sababu amepata mtaji wa kununua vitambaa vya kuwashonea wateja wao.
Amesema, pia kimemsaidia kutosumbuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali na kwa siku anapata 15,000 hali inapokuwa nzuri, inapokuwa mbaya anapata 5,000 fedha ambayo inatosha kabisa kuendesha familia yake na watoto wakapata mahitaji muhimu ya shule
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED