Malalamiko kwa MSD yamepungua kabisa - DC Kitwale

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:52 AM Apr 30 2025
Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Deusdedith Kitwale

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Deusdedith Kitwale ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tabora, kwa kuboresha na kuimarisha huduma zake Mkoani humo, hali iliyowezesha kupungua kwa malalamiko ya wateja na wananchi kwa ujumla.

Kitwale amewapongeza watumishi wa MSD Kanda ya Tabora, kwa utendaji mzuri, chini ya uongozi wa Meneja Kanda hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Deusdedith Kitwaleha, Rashid Omary na kusema Kanda hiyo imekuwa kiungo muhimu katika kuimarisha huduma za afya, Mkoani humo, ambapo kimkoa upatikanaji  wa bidhaa za afya ni asilimia 89.

Kitwale amesema hayo wakati wa kikao kazi cha wadau wa Tabora wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Tabora, na kusema kuwa inapendeza kuona  malalamiko ya ukosefu wa dawa kwenye mikutano ya hadhara yamepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo ni ishara kwamba huduma hivi sasa zimeimarishwa.

"Niwapongeze MSD kwa utaratibu huu wa kukutana na wateja wake Ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mnyororo wa bidhaa za afya nchini." alisema Kitwale