Katika mwaka 2024/25, mafundi umeme waliosajiliwa na kupatiwa leseni na EWURA wamefikia 6,614 mwaka 2025 kutoka mafundi 2,751 mwaka 2020/21 sawa na ongezeko la asilimia 240. Leseni hizo hutolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (a) na 8 (1) cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131.
Aidha, leseni 1,378 za mafundi umeme zilitolewa ikilinganishwa na leseni 1,265 mwaka 2023/24 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 9. Kati ya waliopewa leseni, 1,334 ni wanaume na 44 ni wanawake.
Utoaji wa leseni hizo umesaidia kuwapata mafundi wenye ujuzi wa uwekaji wa mifumo bora ya umeme na salama kwa wananchi, hususan maeneo ya vijijini. Mchanganuo wa leseni hizo ni kama ifuatavyo:
(i) Leseni 69 za daraja “A” zimetolewa kwa wataalam wenye ujuzi wa kufunga mifumo ya umeme hadi kiwango cha msongo wa kilovoti 400;
(ii) Leseni 97 za daraja “B” zimetolewa kwa wataalam wenye ujuzi wa kufunga mifumo ya umeme hadi kiwango cha msongo wa kilovoti 33;
(iii) Leseni 778 za daraja “C” zimetolewa kwa wataalam wenye ujuzi wa kufunga mifumo ya umeme hadi kiwango cha msongo wa kilovoti moja (1);
(iv) (iv) Leseni 428 za daraja “D” zimetolewa kwa wataalam wenye ujuzi wa kufunga mifumo ya umeme hadi kiwango cha msongo wa kilovoti 0.23;
(v) (v) Leseni moja (1) ya daraja “S1” imetolewa kwa mtaalam mwenye ujuzi wa kufunga mifumo maalum ya kitaalamu (special work) hadi kiwango cha msongo wa kilovoti 400; na,
(vi) (vi) Leseni tano (5) za daraja “S3” zimetolewa kwa wataalam wenye ujuzi wa kufunga mifumo ya kitaalamu ya umeme (special work) hadi kiwango cha msongo wa kilovoti 1.
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED