Kufikia Aprili 2025, EWURA ilitoa jumla ya vibali 215 vya ujenzi wa miundombinu ya mafuta ambapo vibali 182 vilitolewa kwa vituo vya mjini na vibali 26 kwa vituo vya vijijini.
Aidha, vibali vitano (5) vilitolewa kwa ajili ya miundombinu ya kuhifadhi mafuta kwa watumiaji wakubwa kama vile viwanda na migodi, na vibali viwili (2) kwa ajili ya maghala ya kuhifadhi na kujaza LPG.
Kazi nyingine zilizotekelezwa na EWURA ni kusimamia taratibu za uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini; na kusimamia ubora wa bidhaa za mafuta ambapo jumla ya sampuli 334 kutoka katika vituo vya mafuta na maghala zilipimwa ubora na sampuli 321 sawa na asilimia 96.1 zilikidhi viwango stahiki vya ubora.
Taratibu za kisheria zilichukuliwa kwa vituo ambavyo vilibainika kuwa na mafuta yasiyokidhi viwango vya ubora. Aidha, EWURA ilikagua ubora wa miundombinu 569 ya mafutaambapo miundombinu 451 sawa na asilimia 76.2 ilikidhi viwango vya ubora ikiwemo vigezo vya masuala ya afya, usalama na mazingira.
#Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati 2025/26
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED