Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amegiza kuwa ifikapo Septemba 30, mwaka huu vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambavyo vilikopeshwa fedha na halmashauri zote za mkoa huu vihakikishe vinarejesha mikopo hiyo na baada ya hapo hatua kali zitaanza kuchukuliwa.
Akizungumza leo Juni 17, 2025 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi cha kujadili hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema kama fedha hizo hazitarejeshwa baada ya muda huo Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao walihusika kuidhinisha mikopo ya vikundi hivyo wataaanza kukatwa mishahara yao kufidia mikopo hiyo.
Awali Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Msafiri Peter, amesema zaidi ya Sh.Milioni 146 zilizokopeshwa kwa vikundi 61 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hazijarejeshwa ambapo kutokana na hali hiyo vikundi sita vimechukuliwa hatua kwa kufunguliwa kesi mahakamani na vikundi 55 vimepewa notisi ya kupelekwa mahakamani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED