Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme (ETDCO) iliyopo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekamilisha mradi wa umeme wa grid ya Taifa kutoka Tabora hadi Katavi na baada ya muda wa matazamio umeme huo utafikishwa kwa wananchi ili kutatua changamoto ya kukosa umeme wa uhakika.
Akizungumza wakati wa kupima njia ya upokeaji wa umeme katika kituo cha Mpanda Kaimu Meneja Mkuu ETDCO CPA Sadock Mugendi amesema laini ikotayari kwaajili ya kuingiza umeme ndani ya mkoa wa Katavi nakinachoendelea sasa ni matazamio kwa kipindi cha miezi sita.
Nae kaimu mkurugenzi wa huduma za ufundi ETDCO Mhandisi Dismas Masawe, amesema mradi huo umegharimu kiasi cha sh. bilioni 116.
Kwaupande wao wananchi wa mkoa wa Katavi wamesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza fursa za ajira kutokana na kuongezeka kwa viwanda vitakavyo toa ajira kwa wananchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED