Tanzania yashiriki Mkutano wa Dunia Masuala ya Mawasiliano ya Simu Hispania

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:16 PM Mar 05 2025
Tanzania yashiriki Mkutano wa Dunia Masuala ya Mawasiliano ya Simu Hispania.
Picha: Mpigapicha Wetu
Tanzania yashiriki Mkutano wa Dunia Masuala ya Mawasiliano ya Simu Hispania.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameshiriki katika Mkutano wa Dunia wa Masuala ya Mawasiliano ya Simu (Mobile World Congress 2025) unaofanyika katika mji wa Barcelona, Hispania.

Katika mkutano huo Waziri Silaa amepata nafasi ya kushiriki katika mijadala kwenye masuala ya Ujumuishaji wa uunganisho wa katika mfumo wa mawasiliano na namna ya kukabiliana na changamoto za masafa,  Uboreshaji wa Mifumo ya Usimamizi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USF) katika nchi za Afrika ambapo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote wa Tanzania (UCSAF) umekuwa mfano kati ya mifuko inayoendeshwa kwa uwazi na mafanikio na mada nyingine ilikuwa ni Uwepo wa Bei nafuu za Masafa zinazochochea Usawa.  

Waziri Silaa ametumia mkutano huo kutangaza Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa Tanzania uliozinduliwa 29 Julai 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuhamasisha GSMA kuwakaribisha wanachama wake kushiriki utekelezaji wake.