Urusi na Belarus kuanzisha luteka ya pamoja ya kijeshi

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 02:49 PM Sep 12 2025
Urusi na Belarus kuanzisha luteka ya pamoja ya kijeshi kuonyesha uimara wa majeshi yao.
PICHA: MTANDAO
Urusi na Belarus kuanzisha luteka ya pamoja ya kijeshi kuonyesha uimara wa majeshi yao.

Urusi na Belarus zimeanza luteka ya pamoja ya kijeshi inayojumuisha maelfu ya wanajeshi, hali inayozua wasiwasi upande wa Magharibi. Luteka hiyo inanuiwa kuonyesha ushirikiano wa karibu wa kiulinzi kati ya mataifa hayo.

Luteka hiyo inanuiwa kuonyesha ushirikiano wa karibu wa kiulinzi kati ya mataifa hayo mawili na uwezo mkubwa pia wa Urusi kijeshi, wakati ikiendesha vita vyake vya miaka mitatu na nusu nchini Ukraine.

Zoezi hilo linajiri siku kadhaa baada ya droni za Urusi kurushwa Polandna kuzua wasiwasi kwamba vita vya Urusi na Ukraine vinaweza kutanuka na kuliathiri eneo zima la Ulaya. Jeshi la Urusi hata hivyo lilisema halikuilenga Poland kwa maksudi huku viongozi wa Ulaya wakilielezea tukio hilo kama uchokozi wa wazi.