Mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wananchi kupuuza kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaopinga kura ya mapema, akisisitiza kuwa ni utaratibu wa kisheria.
Akizungumza leo Oktoba 2 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Bubwini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Dk. Mwinyi amesema kura ya mapema ipo kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Zanzibar Namba 4 ya mwaka 2018, ambayo inawaelekeza wasimamizi wa uchaguzi kupiga kura siku moja kabla ya uchaguzi mkuu.
Amesisitiza kuwa wananchi waendelee kuhubiri amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ili taifa liendelee kudumu katika mshikamano na utulivu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED