Kafulila, Dau wateuliwa kuongoza Bodi za UDART, DART

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:57 PM Oct 02 2025
Kafulila, Dau wateuliwa kuongoza Bodi za UDART, DART.
Picha: Mtandao
Kafulila, Dau wateuliwa kuongoza Bodi za UDART, DART.

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika uongozi wa bodi za usimamizi wa huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka kwa kuvunja bodi zilizokuwapo na kuteua viongozi wapya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua David Kafulila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuimarisha ufanisi na uendelevu wa huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.