Wananchi wa Karatu, mkoani Arusha, katika shamrashamra za kumsubiria mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ambaye leo Oktoba 3, 2025, anamalizia kampeni mkoani humo kisha kuelekea Katesh, wilayani Hanang', mkoani Manyara, kuendeleza kunadi sera na ilani ya uchaguzi.
Akiwa mkoani Arusha Samia amefanya mikutano mitatu akinadi sera na ilani ya uchaguzi, huku ahadi zake zikilenga kufungua jiji hilo katika utalii na kuongeza ajira zaidi kwa vijana ambayo ndio nguvu kazi ya taifa katika kukuza uchumi wa nchi.
Agosti 28, 2025, Dk. Samia alizindua kampeni za chama hicho mkoani Dar es Salaam, kisha akaanza kuchanja mbuga kwenda mkoa kwa mkoa akianzia Mkoa wa Morogoro.
Kila mkoa Dk. Samia ametumia fursa za kiuchumi zinazopatikana kila mkoa kueleza namna atakavyozitumia kuleta mabadiliko ya uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi wake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED