Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, ameahidi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza taifa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Singida, Doyo amesema serikali hiyo itakuwa msingi wa kuimarisha mshikamano, maridhiano ya kitaifa na umoja wa Watanzania wote, sambamba na kujenga taifa linaloongozwa kwa misingi ya uadilifu, uwazi na usawa.
Amesema kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, NLD itatoa fursa kwa makundi na vyama mbalimbali kushiriki moja kwa moja katika uongozi wa nchi, jambo litakalowezesha mawazo mapya na ubunifu katika kuliongoza taifa.
“Tunataka Tanzania yenye mshikamano wa jamii. Serikali ya Umoja wa Kitaifa itawaunganisha Watanzania wote bila kujali chama, kabila au dini kwa lengo la kuleta maendeleo ya pamoja. Nchi hii ni yetu sote, na kila mmoja anapaswa kushiriki kulijenga taifa letu,” amesema Doyo.
Kwa mujibu wa maelezo yake, serikali hiyo itakuwa chachu ya kusikiliza sauti za wananchi wote, kuondoa mpasuko wa kisiasa, na kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha wote bila upendeleo.
Aidha, Doyo amebainisha manufaa ya serikali hiyo kuwa ni pamoja na:
Amesisitiza kuwa chama chake, NLD, kimejengwa juu ya misingi ya mshikamano na ushirikiano wa kitaifa, na hivyo kipaumbele hicho ndicho atakachokileta serikalini mara tu baada ya kushinda urais.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED