Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumhoji aliyeandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa “siku za Kitima zinahesabika’ pamoja na watu wote waliohusika na uhalifu huo, kisha kuchukua hatua kali za kisheria.
Pia ameagiza kusakwa na kukamatwa kwa alitetengeneza na kusambaza Waraka Feki wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), kwa kuwa ulilenga kuzua taharuki kwa umma.
Waziri huyo ameyasema hayo jana Mei 2, 2024 mjini Dodoma wakati wa hafla ya kiwaaga watumishi wa umma waliostaafu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
“Naliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta kwa haraka, yule mtu aliye-tweet kwenye mitandao ya kijamii kwamba,” siku za Kitima zinahesabika, na hatua kali za kisheria zichukuliwe haraka iwezekanavyo, kwa watu wote watakaobainika kuhusika katika tukio hilo,"amesema Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe (CCM).
Aidha, amelaani tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Dk. Charles Kitima, lililotokea majira ya saa nne usiku Aprili 30, 2025 katika makao makuu ya TEC, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Aidha, amesema serikali inatambua na kutathimini mchango mkubwa wa dini na tunamuombea Padri Kitima uponyaji wa haraka na kurejea salama katika majukumu yake muhimu kwa taifa.
Pia, amesema ni muhimu wananchi wakapuuza waraka huo feki kwa kuwa walioandaa hawana nia njema na taifa.
Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii mtu aliyetambulika kwa jina la Dk. Frey Edward Cosseny aliandika "Mwambieni Kitima iko siku ataingia kwneye 18 hatokaa asahau Tanzania Muacheni ajifanye mwanasiasa. Mfikishieni message siku si nyingi atapata anachokitafuta dawa yake iko jikoni atakuja kuozea jela"
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED