Bunge la mpongeza Rais Samia kupandisha mshahara

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 04:40 PM May 02 2025
Bunge.
Picha:Mtandao
Bunge.

Bunge limempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kupandisha mshahara kwa kima cha chini kutoka Sh. 370,000 hadi 500,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 35.1.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Mei 2, Mbunge wa Viti Maalum Dk. Alice Kaijage, alisimama kuomba kutoa taarifa kwa Spika wa bunge.

“Taarifa mweshimiwa Spika nasimama kwa kanuni ya 54 naomba kutoa taarifa ya dharura lakini dharura ya pongezi jana katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa ilifanyika mkoni Singida Rais alitoa kauli yake ya kupandisha mshara wa kima cha chini kwa asilimia 35.1.“Licha ya mabilioni ya fedha ambazo amewekeza kwenye ujenzi wa miradi mkubwa lakini pia mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ambao angeutumia kutoa kisingizio lakini yeye ametamka kupandisha mishahara kwa kima cha chini kutoka Sh. 370,000 hadi 500,000 ikiwa ni miaka tisa imepita tangu watumishi wapandishiwe mishahara yao hivyo basi niwaombe wabunge wenzangu waniunge mkono bunge lako limpongeza mweshimiwa Rais,”amesema

Aidha, Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson, akitolea ufafanuzi kuhusu taarifa hiyo ya mbunge amesema kanuni za bunge zinatoa fursa kwa bunge kupongeza pale inapoona ifaa.

“Waheshimiwa wabunge kanuni zetu zinatoa fursa ya kupongeza na mwenzetu mweshimiwa mbunge Dk. Alice Kaijage amesesimama kwa kanuni ya 54, akitoa taarifa ya dharura yakupongeza lakini hivyo kwakua sisi ni wawakilishi wa wananchi hatuna budi kumpongeza Rais kwa kutukio la jana,”amesema