Baadhi ya makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, waliwahi kugombea ubunge pamoja na watiani wa nafasi hiyo wanaopingana na msimamo wa 'No reforms No Election' maarufu kama G-55 wameanza rasmi kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya CHADEMA kutobadili msimamo.
Mzozo mkubwa wa ndani wa makada hao ulibuka kutokana na msimamo wa "No Reforms No Election" unaoongozwa na uongozi wa juu wa chama hicho, msimamo unaodai kuwa hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu kama hakutafanyika mabadiliko ya kimfumo katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba, sheria, na kuhakikisha kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.
Leo Mei 2, 2025 katika Mkutano wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Amos Makalla amepokea makada wawili miongo mwa wale 55 walionekana katika waraka wa kupinga msimamo huo.
Waliopokelewa katika mkutano ni pamoja na mtiasaini namba 37 Andrew Peter Matyoko ambaye alikuwa Mwenyekiti Wilaya na Mkoa wa Mwanza.
Mwingine ni Mtiasaini namba 35 Andrew Massenya ambaye pia alikuwa Mjumbe Kamati ya Kanda Victoria na wote wakiwa watia nia Jimbo la Ilemela.
Pamoja na Wanachama wengine zaidi ya 100 kutoka Wilaya za Kwimba, Misungwi na Sengerema waliopokelewa na CCM ni Kada wa chama hicho Khalid Ausii ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya Kanda Victoria.
Wengine ni Shan Saad, Mjumbe Kamati Tendaji Ilemela, Mjumbe Kamati Tendaji Ilemela Godwin Kagame.
Akizungumza mara ya kupokea makada hao Makalla amewawaagiza Makatibu WA CCM kutoka Wilaya husika kuhakikisha wanafanya utaratibu haraka wa kuwapatia Kadi za chama hicho.
"Baada ya kupata kadi hizo mtakuwa tayari wanachama halali wa CCM na mtakuwa na haki ya kupata stahiki zote za wanachama wa CCM," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED