Ujenzi wa Meli ya MV Mwanza wafikia asilimia 98

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:27 PM May 02 2025
news
Marco Maduhu
Meli ya MV Mwanza

UJENZI wa Meli ya MV Mwanza,umefikia asilimia 98, huku ikitarajiwa kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yamebainishwa leo Mei 2,2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa,wakati alipotembelea mradi huo akiwa na Waandishi wa Habari kutoka Shinyanga na Mwanza.

Amesema wakati Rais Samia anaingia Madarakani, alikuta ujenzi wa Meli hiyo upo asilimia 33,lakini sasa hivi umeshafika asilimia 98,na gharama zake ni sh.bilioni 138.

"Meli hii itakuwa ikisafiri safari za ndani na nje ya nchi, na itachochea ukuzaji wa uchumi wa nchi,"amesema Msigwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (TASHIKO), Neema Mwale, amesema ujenzi wa Meli hiyo ulianza 2019 na utakamilika Mei mwaka huu.

Amesema Meli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 12,000,pamoja na mizigo Tan 400.