Askofu Ruwa’ichi: Kanisa Katoliki halina ugomvi na serikali

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:19 PM Oct 01 2025
Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi

Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi, amesema Kanisa Katoliki halina ugomvi wowote na serikali na halina mpango wa kupigana nayo mieleka.Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa Misa ya Jubilei ya Mapadri wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria, Msimbazi Centre, Askofu Ruwa’ichi alisema kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinazolenga kulichafua Kanisa.