Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limethibitisha kumshikilia bondia maarufu, Hassan Mwakinyo (29), kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally (21), mvuvi na mkazi wa Sahare, jijini Tanga, baada ya kumtuhumu kuwa ni mwizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa Mwakinyo anahusishwa na tukio hilo, ambalo lilitokea wakati mvuvi huyo alipokuwa akipita karibu na makazi ya bondia huyo.
"Uchunguzi wa tukio hili unaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya kukamilika. Aidha, hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani," amesema Kamanda Mchunguzi.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu huku uchunguzi ukiendelea, na kuwasihi kuepuka kujichukulia sheria mkononi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED