Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akimwakilisha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kutoa salamu za pole, amesisitiza umuhimu wa kuthamini na kutambua mchango wa viongozi kabla ya kufariki dunia.
Amesema ni vyema maneno mazuri yanayosemwa sasa kuhusu Prof. Philemon Sarungi yangefanyika wakati wa uhai wake, ili aondoke akiwa na amani. Chalamila amehoji mantiki ya kupendekeza jina la Prof. Sarungi litumike kwa Taasisi ya MOI baada ya kifo chake, akisema hatua hiyo ingefaa kufanyika mapema ili kumuenzi alipokuwa hai.
Aidha, amewakumbusha watu kuwa Prof. Sarungi aliishi hadi umri wa miaka 90 karibu wote akiwa kwenye kiti cha magurudumu (wheelchair), lakini wengi hawakuwahi kumtembelea. "Ni muhimu kufanya mambo haya kabla mtu hajafariki," alihitimisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED