CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa NEC, Organnaizesheni, Issa Haji Ussi, umamuzi huo ulifikiwa Machi 10, mwaka huu na kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
“Ukomo huo utaanza kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2030,”imesema tarifa hiyo.
Aidha, imefafanua kuwa kikao hicho kilikuwa na agenda mbili ya mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola toleo la 2022, na rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED