MTOTO WA OSAMA BIN LADEN; Asimulia yasiyojulikana kumhusu baba yake

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 05:02 PM Mar 11 2025
Osama bin Laden
Picha: Mtandao
Osama bin Laden

"MAISHA kama mtoto wa Osama bin Laden ni magumu sana. Hata leo, watu wanaogopa kushirikiana na sisi," anasema…

Ni kauli ya mtoto wa Osama bin Laden, Omar bin Laden, akisimulia taswira ya baba yake, na athari aliyoiacha hadi leo kijamii.

Makala haya yanaangazia maisha ya Osama bin Laden kutokana na taarifa kutoka kwa mwanawe, makamanda wa zamani wa Afghanistan na jamaa zake.

Tathmini hii ni jinsi mvulana mwenye haya au mtulivu alivyobadilika na kuwa mwenye msimamo mkali ambaye alitafutwa na mashirika mengi ya kijasusi kwa miaka mingi.

Imesimuliwa na mwanawe Omar, anayeishi huko Ufaransa.

Mtoto wa Osama bin Laden, Omar bin Laden,
Mtoto wa Osama bin Laden, Omar bin Laden, anayeishi Ufaransa, anasema baba yake alikuwa "kama babu yetu." 

Mara nyingi, alikuwa mpole, lakini wakati mwingine alikasirika na kuwa mkali sana, kwa sababu maisha yake mwenyewe yalikuwa magumu kweli.

Omar bin Laden, anasema baba yake hakujulikana hadi miaka ya 1990 na "hakuwa na mawasiliano na familia yake katika nchi yangu (Saudi Arabia) baada ya vita vya Sovieti."

"Familia ya bin Laden walijaribu kutojiingiza katika matatizo yoyote na mfalme wa Saudia au familia ya kifalme."

Omar anasema kuna kipindi aliwahi kuishi nchini Afghanistan na baba yake. Anasema kuwa yeye na mama yake, Najoo Ghanem, waliondoka Afghanistan baada ya mashambulizi ya Septemba 11.

"Sikuwa na nia ya kutaka vita vikubwa na Marekani." Sikutaka hilo, hivyo basi niliamua kuondoka na kumwomba baba ruhusa. Hakutaka niondoke, lakini hatimaye aliniruhusu."

Maisha ni magumu kama watoto wa Osama bin Laden, na hata leo, watu wanahisi aina fulani ya hofu wanapotuona," Omar anasema

Ilikuwa mwaka 1971 na alikuwa akiishi Oxford, Uingereza, akifanya kozi ya lugha ya Kiingereza. 

Kijana huyu anatoka moja ya familia tajiri zaidi nchini Saudi Arabia, ambayo pia ilikuwa na uhusiano wa karibu na familia ya kifalme ya Saudia.

Mwanamke wa Kihispania ambaye alikutana na Osama na ndugu zake wengine wawili wakati huo alisema miongo kadhaa baadaye kwamba, Osama alionekana kuwa na akili sana akiwa na umri mdogo, lakini hakuwa anavutiwa sana na dini au siasa.

HUYU NDIYE OSAMA

Osama bin Laden, alizaliwa Machi 10, 1957. Ni miaka 69 iliyopita huko, nchini Saudi Arabia. 

Alikuwa mvulana mwenye aibu tangu akiwa mdogo Marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza.

Lakini baada ya matukio ya mwaka wa 2001 huko Marekani na kama kiongozi wa shirika la kimataifa la watu wenye msimamo mkali la Al-Qaeda, alijulikana sana duniani kote.

Miaka 10 baada kuuawa karibu watu 3,000 katika tukio hilo, Osama bin Laden aliuawa katika uvamizi wa wanajeshi wa Marekani huko Abbottabad, Pakistan.

Mwaka 2002, Makala ya BBC iliyoitwa "Meet Osama," iliangazia watu waliomwona Osama akiwa mvulana. Brian Fayfield-Shuyler, mwalimu katika shule ya wasomi ya Saudia huko Jeddah, alisema Osama alikuwa na haya na hakuzungumza sana "watoto wengine wa Saudi waliniomba nibadili dini kuwa Mwislamu, lakini Osama hakuwa mmoja wao, sio ambaye alikuwa maarufu darasani."

Anasema kuwa Osama alikuwa na hamu kubwa ya kujifunza Kiingereza, lakini pia alipenda sana masuala ya dini. 

Mwalimu huyo wa Kiingereza anasema kwamba baadhi ya ndugu wa kambo wa Osama walikuwa wamesoma nje ya nchi na walizoea maisha ya nchi za Magharibi, lakini Osama hakuwa hivyo.

Osama alisoma katika chuo kikuu cha Jeddah, Saudi Arabia, ambako alikutana na maprofesa wenye msimamo mkali.

Osama alisomea uhandisi wa ujenzi katika Chuo Kikuu cha King Abdulaziz huko Jeddah, na mawazo yake yalibadilika wakati akiwa mwanafunzi.

Mamake Osama bin Laden, Ayla Ghanem, alionekana hadharani kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018, na kuliambia gazeti la The Guardian kwamba mwanawe alibadilishwa na kuwa mwenye itikadi kali alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha King Abdulaziz. 

"Watu walimbadilisha akiwa chuo kikuu, akawa mtu tofauti kabisa," alisema.

Osama bin Laden alikutana na Abdullah Azzam, mwanachama wa Muslim Brotherhood, miongoni mwa watu wengine akiwa chuo kikuu. Abdullah Azzam alifukuzwa Saudi Arabia kwa shughuli hizi, lakini baadaye akawa chanzo cha msukumo kwa Osama.

Mama yake Osama, akikumbuka wakati huo, alisema, "Osama alikutana na baadhi ya watu ambao walibadilisha mawazo yake. 

Unaweza kuwaita madhehebu ya kidini. Walikuwa wakipata pesa kwa madhumuni yao wenyewe. Mara zote nilimkanya akae mbali na watu hawa, lakini hakusema kuhusu shughuli zake."

Osama bin Laden alikwenda Afghanistan kupigana na vikosi vya Sovieti katika miaka ya 1980. 

"Alifuja mali yake yote nchini Afghanistan na kwenda huko kwa kisingizio cha kufanya biashara ya familia," anasema mamake Osama, Ayla Ghanem.

Osama bin Laden alikuwa akiwasaidia Mujahidina wa Afghanistan kupitia utajiri wake binafsi, lakini baadhi ya makamanda wa Mujahidina hawakujua hilo.

Akizungumza katika makala ya BBC kwa jina "Bin Laden: The Road to 9/11", kamanda wa zamani wa mujahidina Abdullah Anas alisema kuwa, Osama bin Laden pia alikwenda Afghanistan na wahandisi kadhaa ambao walikuwa wakishirikiana na kampuni ya ujenzi ya familia yake huko Jeddah.

Rafiki yake na kamanda wa Mujahidina huko Afghanistan (Asam Daraz) alifurahia kwamba tajiri kama huyo alishiriki katika vita yeye mwenyewe.

Sayed Wahidyar, kamanda wa zamani wa Mujahidina, anasema kwamba katika miaka ya 1980, Waarabu 12 walijiunga nasi, mmoja wao akiwa Osama..

"Sio kwamba alikuwa nasi kwa siku chache, lakini alikuwa na sisi kwa miezi kadhaa." Sikumbuki haswa ni miezi mingapi, ila alikuwa na sisi kwa miezi sita hadi minane. 

Waliishi huko kama wapiganaji wa kawaida. Ilibidi tuwe wapole kwa Waarabu. "Walikuwa na mapenzi ya dhati lakini hawakuelewa mbinu za vita.

Baada ya kuanza kuishi Afghanistan, bin Laden kwanza alianza kwa kuendesha tingatinga kwenye miradi ya ujenzi kwa madhumuni ya kijihadi. Ujuzi aliokuwa amejifunza katika kampuni ya ujenzi ya familia yake kabla ya kuhamia Afghanistan.

Aliyekuwa kamanda wa mujahidina Abdullah Anas anasema anakumbuka kumuona Osama bin Laden "akiendesha tingatinga" wakati wa safari ya kuelekea kaskazini.

Anasema alipomuuliza Osama alikuwa anafanya nini. Alijibu: “Lazima tuwajengee mujahidina barabara, tuweke zahanati kwenye mapango ya milima."

Sayed Wahidyar anaongeza, "Mwanzoni, Osama hakujua chochote kuhusu jinsi ya kupiga risasi, (lakini) alitutazama kama walimu kujifunza jihadi na vita."

"Alitutazama na kujifunza polepole jinsi ya kutumia silaha," anasema "Alipojifunza kuzitumia, aliingia vitani na sisi."

"Wakati wa mapigano tulilazimika kumwambia akae chini, vinginevyo angepigwa risasi, alishindwa kujizuia na alikimbia kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Hatimaye, nilimwambia kwa hasira, 'Tulia,' naye akafanya hivyo."

Anasema kuwa Osama hakuwa mrefu, alikuwa mwembamba, lakini hakuogopa kupigwa na risasi.

Abdullah Anas anasema kwamba baada ya muda, Osama alibadilika kutoka mtu ambaye alitoa misaada hadi kuwa shujaa.

Khalid Batrafi, rafiki wa utotoni wa Osama bin Laden alisema: "Watu hubadilika, vita hubadilisha watu, na ndivyo ilivyotokea kwa Osama," alisema kwenye kipindi cha "Bin Laden: Road to 9/11" cha BBC Select.

Osama alitiwa moyo na fikra za Mmisri mwenye msimamo mkali Ayman al-Zawahiri (kiongozi wa al-Qaeda na mrithi wa Osama), na wakati Al-Qaeda walipounda jeshi lililoitwa Jihad, Osama alikuwa na jukumu muhimu. 

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Sovieti kutoka Afghanistan, Osama alirudi Saudi Arabia, lakini hakufurahia maisha ya jijini humo.

Mkuu wa kijasusi wa Saudia Turki al-Faisal anasema Osama alimtaka kuwatumia mujahidina kupindua serikali katika nchi jirani ya Yemen. 

"Nilishangaa," anasema Turki Al-Faisal "Nilijua mara moja kwamba kijana huyu mwenye haya ambaye hakuzungumza sana alikuwa amebadilika."

Osama aliondoka Saudi Arabia na kuelekea Sudan mwaka 1991. Huko alihojiwa na mwandishi wa habari wa Marekani Scott McLeod. 

"Alisema mwanamfalme Paul alikuwa mjinga, alimcheka, lilikuwa suala la ugomvi wa kifamilia na kisiasa," Scott MacLeod alisema.

Vita vya Osama havikuwa vya familia ya kifalme ya Saudia pekee. Alipokonywa uraia wa Saudia na kufukuzwa kutoka Sudan. 

Alikuwa amesalia na Afghanistan pekee alikoruhusiwa kuishi na kutoka hapo mpango wake wa jihadi ya kimataifa ukajulikana.

Miaka minne kabla ya shambulio la Septemba 11, Osama bin Laden alimwambia mwandishi wa habari wa Uingereza Robert Fisk katika mahojiano kwamba 

"Namwomba Mungu atupe nguvu ya kuishinda Marekani."

Osama bin Laden aliuawa huko Abbottabad mwaka 2011, lakini mtoto wake Omar bin Laden anasema matatizo yake hayajapungua. 

BBC