Klabu ya Al Ahly imetishia kujitoa kwenye Ligi ya Misri iwapo mechi yao dhidi ya watani wao wa jadi Zamalek itachezeshwa na mwamuzi wa Misri.
Katika ombi la timu hiyo lililotolewa limetaka mwamuzi wa mchezo huo kutoka nje ya nchi ili kuhakikisha usawa zaidi wa kimaamuzi katika mchuano huo.
Kadhalika timu hiyo imeomba kuahirishwa kwa mechi yake dhidi ya mpinzani wake Zamalek katika Ligi Kuu ya Misri, iliyopangwa kuchezwa usiku huu wa Jumanne 11,2024.
Al Ahly wametaka mechi hii kuahirishwa hadi uamuzi wa Chama cha Vilabu vya Kulipwa kufanya mchezo huo na timu ya waamuzi wa kigeni ufuatwe.
Klabu hiyo imesisitiza kwa kauli yake kwamba haitaendelea kwenye kinyang'anyiro hicho endapo matakwa yake ya kutaka mwamuzi kutoka nje ya nchi hayatatekelezwa.
Hatua hii inakuja siku kadhaa baada ya timu ya Simba hapa nchini kususia mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga kwa kile walichodai kuwa ni kuzuiwa na walinzi wa timu hiyo walipohotaji kutekeleza haki yao ya kikanuni ya kufanya mazoezi katika uwanja wa ugenini kabla ya mchezo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED