CCM yamchangia fedha za matibabu kigogo BAWACHA aliyepigwa

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 07:24 PM Mar 28 2025
CCM yamchangia fedha za matibabu kigogo BAWACHA aliyepigwa
Picha:Mpigapicha Wetu
CCM yamchangia fedha za matibabu kigogo BAWACHA aliyepigwa

CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemchangia Sh 1,553, 500 Katibu Mwenezi wa Bawacha Mkoa wa Njombe, Sigrada Mligo, kwa ajili ya kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Peramiho, kutokana na kipigo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, leo akiwa katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa, alitangaza harambee kwaa wanachama CCM kumchagia matibabu kiongozi huyo wa CHADEMA ili akatibiwe zaidi.

Akizungumza na wananchi, CPA Makalla ambaye yupo katika ziara ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya na Iringa, amesema kwa upande wake, amewasiliana na Sigrada wa njia ya simu  na kumpa pole.

Amesema wakati akizungumza naye alimweleza anatakiwa kwenda kufanya matibabu katika Hospital ya Peramiho.

CPA Makalla ametangaza.katika mkutano huo kuwa Sigrada anahitaji msaada ili aweze kujiuguza na kutibiwa na kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida na kuomba michango kwa wanachama wa CCM.

“Mimi ninawaomba hapa tuanzishe mchango wa kumchangia Sigrada kwa ajili ya matibabu yake aendelee kujiuguza ameniambia anaenda karantini nimemwezesha lakini lazima tuendelee kumchangia,” amesema CPA Makalla.

Katika harambee hiyo Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Iringa, Salim Abri amechangia kiasi cha Sh. milioni moja na Sh. 553,500 zimepatikana kutokana na michango iliyotolewa na wana CCM katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Jana, akiwa katika mkutano wa hadhara Mbeya, CPA Makalla  alitoa pole kwa Sigrada na kukitaka chama chake katika Mkoa wa Njombe kwenda kumtembelea.