Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kinafuatilia kwa karibu tuhuma zilizozagaa mitandaoni kuhusu madai ya kupigwa kwa Sigrada Mligo, Mratibu wa Uenezi wa Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA).
Katika taarifa iliyotolewa leo, Machi 31, 2025, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA,Brenda Rupia, chama hicho kimesema kuwa kinalichunguza tukio hilo ili kubaini ukweli na kuchukua hatua zinazostahili kulingana na miongozo ya chama.
Pia, CHADEMA imesema itachukua jukumu la kufuatilia kile kilichokiita njama za Chama cha Mapinduzi (CCM), zinazodaiwa kutumika kama njia ya manufaa binafsi kutokana na tukio la kupigwa kwa Mligo.
Katika taarifa hiyo,CHADEMA pia imeutaka Mratibu huyo kuwa makini na mahusiano yake na CCM, ili kuepuka kutumika kwa malengo yasiyokuwa na nia njema ambayo yanaweza kuathiri si tu hadhi ya chama bali pia hadhi na usalama wake binafsi kama kiongozi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED