KIONGOZI wa kijeshi Min Aung Hlaing, amesema katika hotuba yake kupitia televisheni ya taifa, leo, kwamba idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi, nchini Myanmar imefikia 2,719.
Idadi ya waliojeruhiwa ni 4,521, huku watu 441 bado hawajulikani walipo.
Min Aung Hlaing, ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka na vifo vinaweza kuvuka 3,000.
Wakati huo huo, katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, mwili mwingine umepatikana kutoka kwenye vifusi vya jengo refu lililoanguka, na kufanya jumla ya watu waliopoteza maisha hapo kufikia 14.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED