Profesa Mohamed Janabi ameainisha uzoefu wake katika sekta ya afya, ushauri kwa jamii, na uongozi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kama vigezo vinavyompa sifa za kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.
Katika mdahalo wa wagombea uliofanyika leo, Aprili 2, 2025, Profesa Janabi – ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MNH na mshauri wa Rais wa Tanzania katika masuala ya afya na lishe – alibainisha pia uwezo wake wa kuvutia ufadhili na mikopo nafuu kwa maendeleo ya sekta ya afya.
Nafasi hiyo ya WHO Afrika imebaki wazi kufuatia kifo cha Dk. Faustine Ndugulile kilichotokea Novemba 27, 2024. Mdahalo huu unatoa fursa kwa wagombea kueleza mipango yao katika kuboresha huduma za afya barani Afrika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED