Mkulima ashikiliwa tuhuma za mauaji ya mdeni wake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:11 PM Apr 02 2025
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama.
Picha: Mtandao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Jackson Nestory Katabi (30), mkulima mkazi wa Kaporo, kata ya Kibaoni, wilayani Kilombero, kwa tuhuma za kumuua George Magnus Kayega (30).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 28, 2025, ambapo ugomvi ulizuka baada ya marehemu kukataa kulipa deni la shilingi 1,000 alilokuwa anadaiwa na mtuhumiwa.  

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili.