Fisi wamevamia na kuua kondoo 21, huku wengine tisa wakiwa hawajulikani walipo, katika tukio lililotokea mtaa wa Mahina, kata ya Somanda, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, amesema kuwa msako mkali utaanza mara moja ili kuwanasa fisi hao. Aidha, amewataka watu wote wanaofuga fisi kujisalimisha mara moja kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Tukio hilo limezua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku mamlaka zikiendelea kuchukua hatua za kudhibiti wanyama hao hatari.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED