TikTok huenda ikafungiwa Marekani ifikapo Aprili 5

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:41 PM Apr 02 2025
Mtandao wa TikTok
Picha: Mtandao
Mtandao wa TikTok

Mtandao wa TikTok uko hatarini kufungiwa nchini Marekani kufikia Aprili 5, endapo makubaliano ya uuzaji wake hayatafikiwa.

Serikali ya Marekani inasisitiza kuwa kampuni mama ya TikTok, ByteDance, lazima iiuze kwa kampuni ya Marekani ili kuepuka marufuku hiyo.

Tayari wafanyabiashara wakubwa na kampuni za teknolojia, wakiwemo wawekezaji mashuhuri kama MrBeast, wameonyesha nia ya kuinunua TikTok kwa dau la mabilioni ya dola.

White House ina matumaini kuwa suluhisho litapatikana kabla ya muda kuisha. Hata hivyo, iwapo makubaliano hayatafikiwa, sheria inayoruhusu kupigwa marufuku kwa TikTok nchini Marekani inaweza kuanza kutekelezwa.