Aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Mbeya, Lucia Sulle, ameaga dunia baada ya kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 36.
Sulle alihusika katika ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 25 Februari 2025, wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Fadhili Maganya. Kifo chake kinafikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo kuwa sita (6), wakiwemo waandishi wa habari wawili.
Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Christopher Uhaghile, amethibitisha taarifa ya kifo chake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED