Jamii nchini Myanmar inaendelea kuomboleza baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 2,700, wakiwemo watoto 50 waliokuwa katika shule ya awali karibu na Jiji la Mandalay.
Katikati ya juhudi za uokoaji, Idara ya Zimamoto nchini humo ilitangaza kuwa waokoaji walifanikiwa kumuokoa mwanamke mwenye umri wa miaka 63 kutoka kwenye kifusi cha jengo siku ya Jumanne, ikiwa ni saa 91 tangu tetemeko hilo kutokea.
Tetemeko hilo, lenye ukubwa wa 7.7 katika kipimo cha Richter, lilitokea Ijumaa mchana na linatajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Myanmar katika kipindi cha zaidi ya karne moja, likisababisha kuanguka kwa majengo ya kale na mapya.
Kiongozi wa kijeshi wa Myanmar, Jenerali Mkuu Min Aung Hlaing, akizungumza kupitia televisheni leo Jumanne, Aprili 1, 2025, amesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha imefikia 2,719 na kuna uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka na kuvuka 3,000.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED