Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kimesema kinakusudia kusimamisha wagombea katika kata na majimbo yote nchini pamoja na nafasi ya urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu.Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMA, Benson Kigaila ameyasema hayo leo jijini Mbeya kwenye mkutano na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambapo amesema chama hicho kinajiandaa uzindua Ilani ya Uchaguzi Agosti 4, mwaka huu.Vilevile amesema chama hicho kinaendelea na mchakato wa kumpata mgombea urais akisisitiza kuwa wanaandaa kundi la vijana ambao watazunguka nchi nzima kunadi sera za vijana akidai kuwa kundi hilo limesahaulika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED