Tanzania,Misri kupanua wigo wa ushirikiano

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:42 PM Jul 14 2025
Tanzania,Misri kupanua wigo wa ushirikiano
Picha: Mwandishi Wetu
Tanzania,Misri kupanua wigo wa ushirikiano

Pembezoni mwa Mkutano wa 47 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika na Mkutano wa Saba wa Umoja wa Afrika wa Uratibu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri mwenza wa Mambo ya Nje, Uhamiaji, na Wamisri waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Dk. Badr Abdelatty ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Viongozi hao wamejadili mbinu za kuimarisha na kukuza ushirikiano wa Tanzania na Misri pamoja na kuainisha maeneo mbalimbali ya kimkakati ili kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kukuza biashara kati ya Tanzania na utunzaji wa mazingira katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na ushirikiano katika sekta ya anga.

Aidha, wamejadili pia kuongeza ushirikiano katika biashara na kuwepo kwa ubadilishanaji ujuzi kwa wataalamu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii wa mikutano na senta ya afya.

4