Rais wa zamani wa Nigeria, Mahammadu Buhari, anatarajiwa kuzikwa leo, katika mji wake wa alipozaliwa wa Daura katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha TVC.
Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ametangaza siku saba za maombolezo kwa mtangulizi wake, Muhammadu Buhari, ambaye alifariki katika hospitali moja mjini London, jana.
Buhari alikuwa amekwenda kupata matibabu nchini, Uingereza kwa ugonjwa ambao haujabainishwa.
Tinubu amesema serikali itamheshimu Buhari, ambaye alikuwa na umri wa miaka 82, kwa mazishi ya serikali.
Alikuwa amestaafu kama rais Mei 2023, baada ya kutumikia muda usiozidi miaka minane unaoruhusiwa na katiba.
Hapo awali aliiongoza Nigeria kwa miezi 20, baada ya kuchukua madaraka katika mapinduzi ya kijeshi mnamo 1984, lakini alipinduliwa mwaka uliofuata.
CHANZO: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED