Dk. Mwinyi aongoza dua kumkumbuka Mzee Rukhsa

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 02:52 PM Oct 02 2025
Dk. Mwinyi aongoza dua kumkumbuka Mzee Rukhsa
Picha:Mpigapicha Wetu
Dk. Mwinyi aongoza dua kumkumbuka Mzee Rukhsa

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na wananchi katika dua maalum ya kumuombea Rais wa pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi (Mzee Rukhsa), iliyofanyika leo kijijini Mangapwani, Kaskazini Unguja, alipozikwa kiongozi huyo.

Dua hiyo iliyoongozwa na Ofisi ya Mufti Zanzibar ilihudhuriwa na familia pamoja na viongozi mbalimbali, ambapo pia Dk. Mwinyi alizuru kaburi la marehemu.

Shughuli hiyo imelenga kuendeleza kumbukumbu na kutoa heshima kwa kiongozi huyo mashuhuri, anayekumbukwa kwa mchango wake katika mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini.

Mzee Ali Hassan Mwinyi alifariki dunia Februari 29, 2024 jijini Dar es Salaam na kuzikwa Mangapwani, Zanzibar. Aliongoza Tanzania kati ya mwaka 1985 hadi 1995, akihusishwa na kuimarisha uchumi wa soko huria na kulinda amani wakati wa mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi.

1