Dola milioni tisa bandia zadakwa Mwanza

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 11:48 PM Mar 28 2025
news
Picha: Mpigapicha Wetu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa.

JESHI la polisi mkoani Mwanza limesema linawashikilia watu wanane kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia za kigeni 9740 dola za Marekani kila moja ikiwa na thamani ya USD 100 sawa na dola 974,000.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Kamanda Mutafungwa amesema tukio hilo lilibainika Machi Mosi mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo la Kemondo wilayani Nyamagana mkoani hapa.

Amesema jeshi hilo lilipata taarifa juu ya kuwepo kwa watu hao wenye kiasi kikubwa cha fedha bandia za kigeni zenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya Sh,bilioni 2.59.

“Baada ya kupata taarifa hizo tuliandaa mpango kazi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanane wakiwa na noti badia 9740 kila moja ikiwa na thamani ya dola 100 walizotaka kuziingiza kwenye mzunguko wa fedha,” amesema DCP Mutafungwa.

Aidha amwtaja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Frank Mugunga (34) mkaz wa Kagera, Augustino Mambo (32) mfanyabiashara na mkazi wa Dodoma, Lau Wanjara(45) fundi na mkazi wa Ilemela.

Wengine ni pamoja na Isaya Magoti mganga wa kienyeji na mkazi wa Dar es salaam, Cleophas Msaki (40) Mkazi wa Makondeki, Morogoro pamoja na Jeronimo Method mfanyabaishara na Mkazi wa Mkolani Mwanza.