Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 11:24 PM Mar 12 2025
Jiji la Mbeya kugawanywa  kuwa majimbo  mawili  ya uchaguzi
Picha: Mpigapicha Wetu
Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi

OFISA Utumishi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Nicodemus Tindwa, amesema mchakato wa kuligawa Jiji hilo kuwa majimbo mawili ya uchaguzi umekamilika, baada ya wataalamu wa halmashauri kufanya tathmini na kubaini kuwa linakidhi vigezo vinavyotakiwa.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Tindwa, amesema Jiji la Mbeya lina tarafa mbili, kata 36, mitaa 181, na lina ukubwa wa kilomita za mraba 258.8. 

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, linakadiriwa kuwa na wakazi 141,603.

Kutokana na hali hiyo, Jiji la Mbeya litakuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Mbeya Mjini na Jimbo la Uyole.