MAADHIMISHO ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi yanatarajia kufanyika kitaifa katika mkoa wa Singida mwaka huu ambapo yatakahudhuriwa na watu zaidi ya 2,500.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego wakati akizungumza na kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo ya mkoa na kitaifa, alisema kuwa shughuli hiyo itafanyika katika uwanja wa CCM Liti uliopo Manispaa ya Singida.
Alisema kabla ya kilele cha siku hiyo ya Mei Mosi, kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile michezo, utalii wa barabarani lengo likiwa kuwaonesha wageni wataofika Singida wajue kuna utalii gani, kutakuwa na Usiku wa Kuku ( kuku festival), mashindano ya magari, ngoma za asili na mashindano na ngumi.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, alisema kupitia vikao ambavyo wamevifanya kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mkoa wa Singida wanaamini sherehe hiyo itafanyika vizuri na itakuwa ni ya kipekee.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED