Wizara tano kujadili mahitaji ya Umoja wa Walimu Wasio na Ajira

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:06 PM Mar 12 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao kilichoshirikisha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO)
Picha: Mpigapicha Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizara tano kuchambua Makala ya Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO).

Waziri ameyasema hayo Machi 12,2025 mara baada ya kumalizika kikao cha Mawaziri watatu na NETO, baada ya umoja huo kupaza sauti ya kutaka haki kwneye ajira, kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.

Wizara nyingine ni TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekonolojia.

"Nimeelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumisji, Juma Mkomi kuunda timu ya wataalam kutoka wizara hizi ili kuchambua makala hiyo ili tuweza kutimia mapendekezo yao kupata suluhu ya upubgufu wa ajira kw awalimu," amesema.

Simbachawene amesema serikali ina haki ya kumsikiliza kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba na kwa kuzingatia misingi ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.

Ndani ya makala hizo Kuna hoja za NETO ikiwamo mahitaji yao waliyowasilisha kwa maandishi.