Jimbo la Ushetu kumeanza kuchangamka

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 08:02 PM Jun 04 2025
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Simon Makoye Mayengo,ametangaza Rasmi nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ushetu
Picha:Marco Maduhu
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Simon Makoye Mayengo,ametangaza Rasmi nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ushetu

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Simon Makoye Mayengo,ametangaza Rasmi nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ushetu lililopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Amebainisha hayo leo Juni 4,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema ameamua kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo la Ushetu,baada ya kuona Mbunge aliyepo hatoshi,kutokana na wananchi kukosa maendeleo na kutokuwa na uwakilishi sahihi.

“Mimi kama mwana Ushetu leo natamka Rasmi nimetia nia ya kuutaka Ubunge Jimbo la Ushetu,tuna kwenda kuikomboa Ushetu,sababu Mbunge aliyepo hatoshi,tunataka tuitengeneze Ushetu Mpya kama tulivyo kuwa nayo zamani, kwani ndani ya miaka mitatu wananchi hawajatendewa haki hakuna maendeleo kabisa,”amesema Mayengo.

Aidha,amesema Wabunge wote waliopita kila mtu amefanya kazi pamoja na Mbunge ambaye yupo kwa sasa anaye malizia muda wake,lakini Jimbo kwa sasa lina hitaji Mwakilishi sahihi,ambaye anajali maslahi ya wananchi na kuwaletea maendeleo. 

Katika hatua nyingine ametaja vipaumbele vyake endapo akipata ridhaa ya kuwa Mbunge, kuwa ni kukamilisha ujenzi wa Maboma ya Zahanati ambayo yaliachwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo James Limbeli hayajaezekwa,kuunganisha Kata kwa miundombinu ya barabara,kupeleka umeme vijijini kwa kufika vijiji vyote  na kwamba yeye atakuwa Mbunge wa Vitendo na siyo maneno.

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Simon Makoye Mayengo,ametangaza Rasmi nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ushetu.

Amezungumzia pia suala la kunyanyua zao la Tumbaku, kwamba ataishauri serikali itengeneze mfumo mzuri kupitia KACU kuwa mtu akitaka kujiunga kwenye ushirika,kuwa akishindwa kulipa deni kwenye ushirika Y asikope ushirika X ili kupunguza mandeni ambayo yameshindikana kulipwa kupitia ushirika.

Katika hatua nyingine Mayengo amesema kwamba,tayari ameshapeleka barua kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo ya kupisha uteuzi kwa ajili ya wagombea, kwa nafasi yake ya Mjumbe wa Kamati ya siasa CCM Mkoa, sababu na yeye ni mtia nia.

Amesema kwa maelekezo yaliyotolewa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwamba viongozi wote wenye nyazifa za uteuzi, kamati za siasa,na utekelezaji wilaya na mkoa wanatakiwa kuandika baraua kupisha uteuzi wa wagombea utakao fanyika Julai mara baada ya Baraza la Madiwani na Bunge Kuvunjwa na sasa amesha andika barua hiyo.