Kamati ya Bunge yabaini upungufu mkubwa wa vyoo kwenye shule

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:11 PM Apr 17 2025
Kamati ya Bunge yabaini upungufu mkubwa wa vyoo kwenye shule
Picha: Mtandao
Kamati ya Bunge yabaini upungufu mkubwa wa vyoo kwenye shule

Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imebaini kuna upungufu mkubwa wa matundu vya vyoo katika shule za msingi na sekondari hali ambayo si nzuri kwa ustawi wa Taifa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Justin Nyamoga ameyasema hayo alipokuwa akisoma bungeni maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka 2025/26.

“Serikali ifanya tathmini ili kubaini ukubwa wa tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo katika shule zake zote za msingi na sekondari nchni. Serikali ifanye tathmini ya ubora wa vyoo katika shule zake zote za msingi na sekonda nchini (hasa kwenye shule kongwe),”amesema. 


Ameshauri pia Serikali iweke mkakati wa kumaliza kabisa tatizo la vyoo katika shule zake za msingi na sekondari nchini. 

 Aidha, amesema kila mkoa na halmashauri zake zote zenye upungufu wa vyoo zisimamiwe kwa kuweka mkakati wa kutatua na kukomesha kabisa tatizo laa ukosefu pamoja na ubora hafifu wa vyoo katika shule zake za msingi na sekondari nchini.

 Hata hivyo, katika bajeti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI 2025/26, serikali imepanga kujenga matundu ya vyoo 19,095.