KAMATi ya Bodi ya ya Uwekezaji na Fedha ya Watumishi Housing Investment, imekagua mradi wa Nyumba 101 zinazojengwa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Celestine Muganga, amesema wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo, unavyoendelea, hatua ambayo inaonyesha juhudi za kufanikisha lengo lilowekwa na kuwawezesha watumishi wa umma kumiliki nyumba bora zinazojengwa chini ya WHI.
Meneja Maimamizi.wa mradi huo Msanigu ujenzi Yusuph Mlimakifi amesema hadi Sasa mradi huo umefika asilimia.20 ulianza Seotemba 2024 unapaswa kukamilika Machi 2026.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa WHI, Sefania Solomon, amesema wamekusudia kuendelea kutekeleza miradi mingine kadhaa katika maeneo tofauti nchini, ili kufanikisha watumishi wa umma wenye nia ya kumiliki nyumba.
Mwakilishi ya kampuni ya ujenzi ya kimataifa ya Shadong Hi- Speed Group Wang Younsheng amesema wamekusudia kuhakikisha
Jengo hilo lenye ghorofa 12 linajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na linakamilika kwa wakati.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED