Kigogo CHADEMA atimkia CCM

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 06:35 PM Mar 29 2025
KATIBU wa CHADEMA Jimbo la Iringa, Paschal Chibala akipokewa na Katibu  wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla akihamia katika chama hicho.
PICHA: ROMANA MALLYA
KATIBU wa CHADEMA Jimbo la Iringa, Paschal Chibala akipokewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla akihamia katika chama hicho.

KATIBU wa CHADEMA Jimbo la Iringa, Paschal Chibala, ametangaza sababu zilizomfanya kuhama chama chake na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Chibala ametangaza leo kuhamia CCM wakati wa  mkutano wa hadhara wa Katibu  wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, ambaye amehitimisha ziara yake ya siku tatu  katika mikoa ya Mbeya na Iringa. 

Akizungumza baada ya kupokewa na CPA Makalla katika mkutano huo uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa, mkoani Iringa,  Chibala ametaja sababu ni baada ya kuona alikokuwa hawana sera.

Amedai kuwa CHADEMA wanatembea kwa kuwadanganya wananchi no reform.

Kadhalika ametaja sababu nyingine  ni wakati Mchungaji Peter Msigwa, akiwa CHADEMA alimpelekea Mwenyekiti ambaye anadai  hajui kusoma wakati yeye ana Degree (Shahada).