Makalla aishangaa CHADEMA msimamo kuhusu uchaguzi

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 06:05 PM Mar 29 2025
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla
PICHA: ROMANA MALLYA
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amewaambia Watanzania kuwa mwaka huu watasikia mengi kwa sababu, wanaosema hawatashiriki uchaguzi, wanatangaza wakiingia madarakani watakomesha Bet.

CPA Makalla ameyasema hayo leo katika uwanja wa Mwembetogwa, Iringa wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya Na Iringa.

“Wakija kesho hapa muwaulize Ibara ya nne ya katiba yao inasemaje,  hawatasema, wameshaikanyaga katiba yao. CCM ni chama imara kinajali, hakiwezi kuacha kuheshimu katiba.Mgombea Urais tunaye, mgombea mwenza mapema tumempata hayo ndiyo yanawapa hofu. Mkiwauliza mgombea Urais kwao ni nani hawajui. Waziri wa Fedha ni nani pale mnayemjua?"

CPA Makalla amesisitiza kuwa CHADEMA hakijajipanga na uchaguzi kwa kuwa  hawana fedha, wana mgogoro.

“Simliona kule Njombe kilichomtokea Katibu Mwenezi wa Bawacha Mkoa wa Njombe, Sigrada Mligo,  leo nimeongea naye na nimemtumia Sh. milioni 1.6, fedha za harambee iliyofanyika Mafinga (jana), kumsaidia matibabu yake ,” anasema.

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa anasema Rais Samia Suluhu Hassn alipokabidhiwa nchi upinzani ukasema hawezi, lakini amefanya mambo makubwa na nchi imepaa.