Makalla:Nipo tayari kubeba matusi

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 07:13 PM Mar 29 2025
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla.
PICHA: ROMANA MALLYA
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla.

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema yupo tayari kubeba matusi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kukitetea na kuwa na chama ambacho kinakubalika kwa wananchi.

CPA Makalla ameyasema hayo leo katika uwanja wa Mwembetogwa, Iringa wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya Na Iringa.

“Sisi tunawaacha kesho mfurahie vituko, lakini ninajua mkutano wao  kesho utakuwa ni kumtukana tu Makalla. 

“Niko tayari kubeba matusi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini kukitetea na kuwa na chama ambacho kinakubalika kwa wananchi kuwapelekea sera nzuri za CCM hiyo ndiyo kazi ya uenezi,

“Leteni tu mawe nipo tayari na kesho mtashuhudia Makalla, kama watawaudhi kaeni nyumbani lakini ninajua habari ya kesho ni hiyo na mimi nipo tayari kwa sababu ndo kazi yangu hiyo,” alisema. 

Makalla aliwaambia wananchi endapo watakuja na no reform, tayari ameshaeleza mabadiliko mengi yaliyofanywa.