MARBURG; WHO yaisifu Tanzania kumaliza kesi ugonjwa huo

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 04:06 PM Mar 13 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus
Picha: Mtandao
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus

TANZANIA leo, imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg, baada ya kutoripotiwa kwa kesi mpya kwa zaidi ya siku 42 tangu kifo cha mgonjwa wa mwisho, aliyethibitishwa Januari 28, mwaka huu.

Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), na kwamba mlipuko huo ambao ulisababisha kesi mbili zilizothibitishwa na zingine nane zinazoshukiwa (wote walifariki), ulikuwa wa pili kutokea nchini.

MARBURG; WHO yaisifu Tanzania kumaliza kesi ugonjwa huo
“Ninatoa shukrani zangu kwa wahudumu wa afya waliokuwa mstari wa mbele, serikali na wenzangu wa WHO_Tanzania kwa kazi yao isiyochoka katika kudhibiti mlipuko huu," Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus katika ukurasa wake wa X.

Mlipuko huo, uliitangazwa Januari 20, 2025 na ule wa mwaka 2023, yote ilitokea katika mkoa wa Kagera, kaskazini mashariki mwa Tanzania.