PSSSF kulipa pesheni kila mwezi Sh.bilioni 70 kukuza uchumi wa nchi

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 07:16 PM Mar 14 2025
Ofisa sheria Mkuu wa PSSSF Valentino Maganga akizungumza na wajumbe wa Misa Tanzania na wadau wa habari wakati wa kikao cha Misa-Wadau, iliyofanyika leo Dodoma.
Picha: Shaban Njia
Ofisa sheria Mkuu wa PSSSF Valentino Maganga akizungumza na wajumbe wa Misa Tanzania na wadau wa habari wakati wa kikao cha Misa-Wadau, iliyofanyika leo Dodoma.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (PSSSF) umetangaza ongezeko la kipimo cha maendeleo ya uchumi nchini kutoka asilimia 22 mwaka 2023 hadi asilimia 36 kwa mwaka 2024/2025.

Akizungumza jijini Dodoma katika mkutano wa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) na wadau, Ofisa Sheria Mkuu wa PSSSF, Valentino Maganga, amesema ongezeko hilo linaelekea kufikia lengo la asilimia 40 iliyopendekezwa kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Maganga amebainisha kuwa thamani ya uwekezaji wa mfuko huo imeongezeka kutoka trilioni 6 hadi trilioni 10, jambo linalochangia maendeleo ya kiuchumi. Pia, alieleza kuwa thamani ya dhamana za uwekezaji katika taasisi za kifedha, majumba, na maeneo mengine imefikia trilioni 9, mchango muhimu katika kukuza pato la taifa.

Aidha, Maganga amesema PSSSF inalipa pensheni ya Shilingi bilioni 70 kila mwezi, na kwa mwaka zaidi ya Shilingi bilioni 800, fedha zinazosaidia kuchochea uchumi kupitia uwekezaji na shughuli nyingine za maendeleo.