Mnyika: Wanaolalamika kubaguliwa, waliomba waachwe wapumzike

By Enock Charles , Nipashe
Published at 11:23 AM May 10 2025
John Mnyika
PICHA: MTANDAO
John Mnyika

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amewakosoa waliokuwa viongozi wa chama hicho waliotangaza kuachana nacho hivi karibuni kwa kile walichodai ni kubaguliwa ndani ya chama hicho akisema viongozi hao walikataa kukutana na uongozi mpya katika vikao.

Akizungumza na wananchi mkoani Kagera jana, Mnyika amesema baada ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika mwezi Januari mwaka huu waliamua kuitisha vikao na viongozi wastaafu lakini baadhi yao waliwakatalia kufika katika vikao hivyo wakitaka waachwe wapumzike.

Mnyika alieleza kushangazwa kwake na madai ya viongozi hao kwamba wanabaguliwa ndani ya chama hicho akidai walikataa wenyewe kukutana katika vikao.