ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, amesema uamuzi wa ‘No reforms No election’ haukuwa wa Kamati Kuu.
Mrema, ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa X alipojibu maoni ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Rugemeleza Nshala na kudai hoja zake hazina ukweli.
Katika hoja zake Mrema anasema, uongozi mpya unasimamia uamuzi ya vikao vya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu wa chama, ila haujaweka ushahidi wowote ule kwamba kulikuwa na azimio la kuzuia uchaguzi.
Ametaka kama lipo jambo lolote, liwekwe mezani dunia ijue na iwapuuze wote wenye hoja kinzani.
Pili anasema uongozi huo umesema walioshindwa uchaguzi wa ndani ya chama ndio wanaopinga, ila hujasema ukweli kuhusu ambao hawakuwa na upande ndani ya uchaguzi ule na ambao ni wagombea ambao walishawekeza kwenye kata na majimbo ya uchaguzi na walitakiwa kufanya maandalizi tangu Tangazo la Katibu Mkuu la Januari, 2023 akiwa Mwanza alipowataka wagombea wote watie nia ya kugombea na waendelee na maandalizi ya kiuchaguzi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED