Mwalimu: Ndani ya Siku 100 nitarejesha viwanda vya chai

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 01:12 PM Sep 28 2025
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu
PICHA: ELIZABETH ZAYA
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu

Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema ndani ya siku 100 baada ya kuingia Ikulu atarejesha viwanda vya chai nchini.

Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kwenye mji wa Lupembe mkoani Njombe wakati akiendelea na kampeni za kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania ifikapo Oktoba 29 mwaka huu. Amesema nchi yoyote ambayo inaua viwanda tafsiri yake ni kuua ukuaji wa uchumi wa nchi.

"Ukiona viwanda vimekufa ujue uchumi wa nchi husika umekufa na hakuna namna utatengeneza ajira na kuondoa umasikini, duniani kote hakuna nchi inayoweza kutengeneza uchumi wa nchi yake kwa kuua viwanda au bila kuwa na viwanda hivyo."

Amesema endapo wawekezaji watashindwa kuendesha viwanda hivyo, serikali itaendesha yenyewe.